Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu vipindi ya mvua vinavyoendelea katika Mikoa mbalimbali kwamba vinatokana na mgandamizo mdogo wa hewa katika Rasi ya Msumbiji.
Joyce Makwata ni Mchambuzi wa Hali ya Hewa TMA, anasema mgandamizo huo umeweza kuvuta upepo wenye unyevunyevu kutoka maeneo ya magharibi mwa Tanzania hususani katika maeneo ya Misitu ya Congo pamoja na maeneo ya Kaskazini ambapo makutano hayo yamesabahisha mvua katika maeneo mbalimbali.
“Kwa kawaida kipindi hiki cha February hatutarajii kupata vipindi vya mvua kwenye maeneo haya ya Pwani ya kaskazini, Nyanda za Juu kaskazini Mashariki pamoja na ukanda wa ziwa Victoria sababu msimu wa vuli unakua umeisha”
“Hizi mvua za February mara nyingi ni mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa, kwa kifupi mvua hizi zimechangiwa na uwepo wa mgandamizo mdogo wa hewa uliopo kwenye rasi ya Msumbiji”