MDOGO wake marehemu Salum Idd Nyange, Abdul Kambaya, ameibuka na kuanika mapya kuhusu familia hiyo ya marehemu ambayo imekuwa maarufu zaidi baada ya mama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim kumtangaza marehemu Nyange kuwa ndiye baba halali wa mwanaye huyo ambaye ni supastaa Bongo, RISASI JUMAMOSI linakupakulia yote!
TUMSIKILIZE KAMBAYA
Akizungumza na RISASI JUMAMOSI, Kambaya ambaye ni mdogo wake marehemu Nyange kwa maana ni mtoto wa shangazi yake, alianza kwa kueleza kuwa ukoo wao ni mkubwa na wenye heshima zake tofauti na watu wengi wanavyopotosha kwenye mitandao ya kijamii.
“Watu wanapotosha mambo, wanaichukulia familia hii kama familia fulani ndogo au ya kimasikini. Hii familia ni kubwa, inajitambua na ina heshima yake tofauti na wanavyofikiri,” alisema Kambaya.
ATOA HISTORIA
Akianza kusimulia historia ya familia yao, Kambaya alisema, yeye alianza kuishi na marehemu Nyange angali wakiwa wadogo nyumbani kwao mtaa wa Sultan, Morogoro.
Alisema mwaka 1988, marehemu na yeye walihamia jijini Dar na kuanza kufanya biashara ya kuuza mitumba.
“Marehemu Nyange alifikia pale Muhalitani, Tandale. Alijenga mji wake pale na alikuwa mtu maarufu tu pale, alifanya pia biashara ya mchele pale sokoni Tandale,” alisema.
UKUBWA WA FAMILIA
Akizungumzia ukubwa wa familia ya marehemu Nyange, alisema anao wajomba wasiopungua 10 Dar pamoja na kwamba wengine wameshatangulia mbele za haki.
“Huu ni ukoo mkubwa sana. Watu tuna maisha yetu, mimi hapa unavyoniona hivi sasa naishi kwangu Mbweni katika nyumba ya ghorofa (tazama ukurasa wa mbele), labda tuwafafanulie ili waelewe.
“Sisi hatukutaka kuutangazia umma kuhusu jambo hili la Diamond na mama yake kwa sababu tuliamini mhusika mkuu ni mama Diamond mwenyewe.
“Sasa kwa kuwa mwenyewe amesema, tunaheshimu kauli yake nadhani sasa Watanzania wenyewe watakuwa wameshasikia kile ambacho amekizungumza maana yeye ndio mama na bahati nzuri hata Diamond mwenyewe naye amekazia hoja ya mama yake,” alisema.
Kwenye mahojiano aliyoyafanya juzi katika Wasafi FM, Diamond alikazia mazungumzo ya awali ya mama yake kwa kusema baba yake halali ni marehemu Salum Idd Nyange.
Alisema, yeye alifahamu jambo hilo mwaka 2000 alipoelezwa na mama yake mkubwa, mama Romy Jones.
TURUDI KWA KAMBAYA
Kambaya alisema, hata marehemu mwenyewe mzee Nyange wakati wa uhai wake, hakuwahi kulizungumza jambo hilo mpaka pale mama Diamond mwenyewe alipoamua kuzunguma jambo hilo kwenye vyombo vya habari.
WANAVYOMFAHAMU DIAMIOND
Alisema, wao kama familia wanamfahamu Diamond siku nyingi kwani alikuwa akihudhuria kwenye shughuli mbalimbali za kifamilia ikiwemo misiba na mambo mengine.
“Nimeshamuona Diamond mara nyingi tu kwenye shughuli za familia. Nimemwona si chini ya mara tatu au mara nne hivi kwenye misiba,” alisema Kambaya.
Alisema hata picha (zipo ukurasa wa mbele) ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni, nyingi zinaonesha dhahiri jinsi ukoo wao ulivyokuwa na ushirikiano kwa muda mrefu.
“Kuna picha ya Nyange inazunguka sana mitandaoni waliikata kutoka kwenye picha yangu ya harusi kwani siku hiyo tulikuwa pamoja na marehemu. Sisi tumeshikana kama ndugu kwa miaka mingi,” alisema Kambaya.
AMTAJA DIAMOND
Alisema hata Diamond mwenyewe alishakuwa karibu siku nyingi na ndugu zake waliozaliwa na Nyange na baadhi yao ameendelea kufanya nao kazi kwa ukaribu hata sasa.
“Hao kina Ricardo Momo, kina Asia ambaye amezaliwa mwaka mmoja na Diamond, wote hao wamekuwa wakiishi kwa kushirikiana kama familia,” alisema Kambaya.
Kambaya alisema, Nyange alifariki dunia 2005 na alizikwa katika Makaburi ya Kijitonyama.
Stori: Erick Evarist
Kwa hiyo Sanura alikuwa wa kuvizia wachuuzi wa Mitumba na Michele kama Lockwole, Anko Amka shosti wa Ezma pia anauza mchele. Danga hachagui.!!
ReplyDeleteSasa na baba yake Mzee Makame Mrisho Kisimba alikuwa mchuuzzi wa nini.?
Mdau, Wauza mchele balaa..!!! Mtoto nae kafata nyayo za mama.
DeleteMsizwa kakimbiwa kaludi Kwa ijuma Mlokole...Hatali hiyooo.
Yule msuka nywele anaitwa nani vile? afanye vinasaba ajue mchezo ukoje
Yule msuka nywele, nanihi alisema ni kuwadi. ngoma dloo.
Deletehukuona gari iliyozawadiwa kaka yake alirudisha hela. pale pale halusini.
Nyange Bubu wanamtegeshea. mwenye mtoto Makame Mrisho Barida..!!! kule Kahama.
DeleteSanura aliipelekesha sana kwa Ukware, je Ezma nae uzi ule ule..?
Kwini Dar lini..!! Jinasue na hawa kina kunguni harufu imechafuka.
Htr
ReplyDelete