WAPINZANI wa Simba kwenye mechi yao ya kimataifa inayotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Mkapa Al Ahly, Waarabu wa Misri wamesema kuwa licha ya joto la Dar kuwa kubwa halitawafanya washindwe kusaka ushindi.
Al Ahly ya Misri ina kibarua cha kusaka ushindi kesho Februari 23 mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Inakumbuka kwamba iliwahi kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ilipocheza na Simba msimu wa 2018, Februari 2019 jambo ambalo linawafanya wawe na tahadhari kubwa licha ya uwekezaji wao mkubwa katika kikosi chao.
Kocha Mkuu wa Al Ahly ya Pitso Mosimame amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya licha ya wapinzani wao kuwa vizuri pamoja na mazingira ya joto la Dar.
"Kwenye mpira jambo ni moja kusaka ushindi ndani ya uwanja, vijana wangu ninatambua wanahitaji ushindi na hilo linawezekana ndani ya uwanja."Watakuwa nyumbani hilo lipo wazi ila nasi pia tuna kazi moja ya kusaka ushindi ndani ya uwanja hakuna namna tupo tayari, licha ya kwamba joto ni kali"