Simba Kuifunga AS Vita ni Uchumi wa Kati





Waziri wa Katiba na Sheria Mwigulu Nchemba, amewaambia Watanzania kwamba wanayo bahati sana kuwa na Rais ambaye usiku na mchana anawaza namna ya kuwaletea maendeleo ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo marais wake hugeuza mahoteli kuwa ofisi zao.

 

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 13, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akizungumza kwa niaba ya waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.

 

 

“Mimi nimezifuatilia sana hizi siasa na nilikuwa ninazipenda tangu nikiwa shule ya msingi, Afrika hapa kupata Rais ambaye masaa 24 kwa wiki, kwa mwaka mzima na kwa awamu nzima anashughulika na maisha ya watu wake tu ni ngumu kumpata, kuna marais wanaongoza nchi wakiwa hotelini na mke wake, wa kwetu akitaka likizo unamuona yuko Chato tu ana anaendelea kuchapa kazi.

 

“Tanzania kuingia uchumi wa kati haikutuma maombi na wala Tanzania kuingia uchumi wa kati haikulipia, ni jambo linalozingatia vigezo na tena vigezo vyenyewe vimezingatiwa na taasisi kubwa zinazoheshimika duniani kama World Bank na IMF.

 

“Kwa wale waliokuwa wanasema kiwango chenyewe tulichofika ni kidogo sana kwanza hawaitendei haki nchi yetu na hawamtendei haki Rais wetu, tulitarajiwa tufike mwaka 2025, lakini tumefika mapema kabla ya muda ule kwa sababu ya ujasiri wa Rais wetu.

 

“Wewe unayepinga kwanini unaona sifa kuitwa maskini?, yaani wenzako wamekuona umeshaondoka kwenye umaskini wewe unajisikia bora zaidi wakuone maskini, angalia nchi inayoweza kutoa Bil. 24 kila mwezi kupeleka elimu kwa watoto wake na bado haijakwama.

 

“Hata jana tu Simba kushinda kule ni uchumi wa kati ndiyo maana hawakuwahi kushinda siku zilizopita, viwango vyao vilikuwa ni vya uchumi wa kati, ninachosisitiza kwamba Tanzania imefikia vigezo vyote,” amesema Waziri Nchemba. Aidha, akizungumzia kuhusu deni la Taifa, Waziri Nchemba amesema kuwa deni bado ni stahimilivu.

 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad