SIMBA na Azam wote kwa pamoja wanatambiana kuelekea mchezo wa leo Jumapili wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.Tambo hizo ni katika kusaka pointi tatu ambapo kila upande unasema: “Hatuwaachi salama, lazima tuwanyoe.
”Wakati mchezo huo ukisubiriwa kwa hamu kuanzia saa 1:00 usiku, itakuwa vita kubwa ya makocha wapya wa timu zote mbili, Didier Gomes upande wa Simba na George Lwandamina wa Azam.
Gomez mrithi wa Sven Vandenbroeck, ana kazi ya kusaka heshima ya kupunguza gepu la pointi dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Yanga wenye 44, huku Simba ikiwa na 32. Tofauti ni pointi 6.
Azam FC chini ya Lwandamina, inahitaji kulipa kisasi cha kunyooshwa na Simba kwenye mechi tatu walizofungwa msimu wa 2019/20.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
Mbili ilikuwa kwenye ligi na moja ya Kombe la Shirikisho.Katika mechi hizo tatu ambazo ni sawa na dakika 270, Azam iliruhusu mabao sita, huku yenyewe ikifunga mawili. Mechi ya kwanza ilifungwa 1-0, kisha 3-2 na ya mwisho 2-0.
Lwandamina amesema kuwa mchezo wa leo una presha kubwa ndani ya uwanja ila wachezaji wake wapo tayari kupambana kusaka ushindi.
Ukiachana na vita ya makocha, pia kuna ishu ya majembe mapya kuoneshana umwamba. Simba wanaye Perfect Chikwende na Taddeo Lwanga ambao wamesajiliwa kwenye dirisha dogo msimu huu.
Upande wa Azam FC, majembe mapya ni Mathias Kigonya, Mpiana Monzinzi na Yahya Zayd, hawa watakuwa na kazi ya kufanya ndani ya uwanja.
Ukiangalia upande wa wakali wa nyavu, Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao nane ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, ana kazi ya kufanya kuongeza mabao kwenye upande wa akaunti yake huku Azam FC mshambuliaji wao Prince Dube mwenye mabao sita na pasi nne za mabao, anatarajiwa kuongoza jahazi lao.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
Kuna nyota watakosekana katika mchezo wa leo, Simba itawakosa Ibrahim Ame ambaye bado hajawa fiti akitokea kwenye majeraha, John Bocco na Erasto Nyoni bado wanasumbuliwa na mejeraha.
Azam nao itawakosa Yakub Mohamed mwenye kadi tatu za njano, Frank Domayo na Abdul Hamahama ni majeruhi.
Kocha Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, amesema: “Lazima tushambulie, hatuwezi kukaa nyuma, tunahitaji kushinda ndiyo maana tumejiandaa kushambulia sana. Hatubaki nyuma kuzuia.
“Simba wana timu nzuri, lakini wana matatizo ambayo tumeyafanyia kazi kuona tunawaadhibu.”Kwa upande wa Gomes, amesema: “Mchezo utakuwa mgumu, lakini tupo tayari kupambana. Ni muhimu sana kushinda.”
REKODI ZAO
Kwenye misimu mitano waliyokutana wakiwa wamecheza mechi 10, Simba imeshinda tano, Azam FC