TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amebadili mbinu ya kuwakabili Halima Mdee na wenzake 18 kuwazuia kuhudhuria vikao vya Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Amesema, Chadema hakitakwenda mahakamani na pia chama hicho hakina polisi wa kuzia ‘wabunge’ hao kuhudhuria vikao vya bunge, badala yake watakwenda kwenye mahakama za umma na za Jumuiya za Kimataifa.
”Hatutakwenda mahakamani, tutapambana kwenye mahakama ya umma wa Watanzania na Mahakama ya Umma ya Jumuiya ya Kimataifa, uwanja wa mapambano ni kubwa sana,” amesema Lissu tarehe 5 Februari 2021, kwenye mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha habari za mtandaoni.
Amesema, Chadema kilichukua hatua stahili kuwatimua waliokuwa wanachama wao kutokana na taratibu zao, na kwamba mamlaka zote za sheria nchini, zimejulishwa kuwa Mdee na wenzake si wanachama wa chama hicho.
Halima Mdee
“Hakuna ubishi kwamba mamlaka za kikatiba zimejulishwa kwamba hawa watu wamefukuzwa uanachama wa Chadema kwa maandishi, vilevile hakuna ubishi wahusika wenyewe wote 19 wamejulishwa kwa maandishi juu ya kufukuzwa kwao.
“…ndio maana wamekata rufaa kwa mujibu wa kanuni husika za chama kwenye Barabza Kuu la chama, wamekata sababu wamejulishwa si wanachama wa Chadema tena,” amesema Lissu.
Na kwamba, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chama kikichukua hatua ya kumfukuza/kuwafukuza wanachama wake, hawana haki ya kuhudhuria vikao vya Bunge.
“Hatutakwenda mahakamani kupoteza muda wetu, tutakachofanya ni hiki cha sasa hivi, kuwaambia Watanzania na dunia kwamba watu wanaoitwa wabunge wa Chadema, hela zenu zinachezewa.
“Sisi hatuna askari wa kuwazuia kuingia bungeni, hatuna uwezo wa kuzuia wasilipwe mishahara na posho, hatuna uwezo wa kufanya wasiitwe wabunge wa Chadema. Kitu ambacho kiko ndani ya mamlaka ya chama ni kuwafukuza uanachama, kujulisha hizo mamlaka za kikatiba kwamba si wanachama wa Chadema,” amsema Lissu ambaye aligombea urais kupitia chama hicho Tanzania Bara na kushika nafasi ya pili.
Amesema, si Spika wa Bunge, Katibu wa Bunge wala mtu yeyota anayepaswa kuwaruhusu Mdee na wenzae kuingia bungeni.
Chadema kupitia Kamati Kuu yake iliyoketi tarehe 27 Novemba 2020, iliwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 kwa kukiuka umauzi wa chama hicho na kwenda kuapishwa bungeni kuwa wabunge wa viti maalumu.
waliotimuliwa Chadema ni Mdee mwenyewe, Ester Bulaya, Esther Matiko, Nusrat Hanje, Grace Tendega na Hawa Mwaifunga.
Wengine ni Jesca Kishoa, Agnesta Lambat, Tunza Malapo, Ceciia Pareso, Asia Mwadin Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza
Loki Dauni inamdatisha huyu mbelijiji. Ya kina Mdee mwachie atumikkie nchi yake. Hhana nchi mbadala kwa gud less na wewe kibeko. Ingia mtanda wa Amazoni utengeneze Euro 3 kwa saa. kuitumia vyema Look dauni.
ReplyDeleteMbinu dumavu kama walio dumaa ki Fikra na medula blongata zao akiwemo huyu KIBEKO Tundu Bovu.
ReplyDeleteWatu wanataka maendeleo na kina mama hawa Majasiri Wanatosha katika kulitumikia Taifa na Wananchi.
Wewe umerudi kwa bwana anasita Damu, hivyo kweli unakula chao BURE..???
Hapa kuna walakini wa jinsia moja anao utetea. Jitathmini mnyampalaa..!!
Oyaa.!! Dakitari ulipo muona virtual visit amekuongezea Dozi au anarekomend
ReplyDeleteupatiwe kitanda cha matibabu ya Mirembe.!!
Mie ningependelea akupunguzie Dozi. Manake ZINAKUCHANGANYA TWUNDU.
GODI LESS YOU.