Tuzo za MTV 2021 za ahirishwa



Tuzo za MTV za muziki wa Afrika ‘MTV Africa Music Awards (MAMAs)’, ambazo zilikuwa zimepangwa kufanyika mjini Kampala mwezi huu zimehairishwa, waandilizi wa tuzo hizo wamesema.

MTV Base Africa imetangaza kupitia mtandao wa Twitter, bila kutoa sababu zilizopelekea kufikiwa kwa uamuzi huo.

“MTV Base inaahirisha Tuzo za muziki wa Afrika 2020. Tutaendelea kuwafahamisha mashabiki kadiri tunavyoendelea kupata taarifa zaidi,” ujumbe huo umesema.

Hivi karibuni, tuzo hizo zimekuwa zikipigwa vita na wanaomuunga mkono Bobi Wine, Jeffrey Smith na Robert Amsterdam, wakitaka waandalizi kufikiria tena uamuzi wao wa kuweka tamasha hilo nchini Uganda.

“Kuandaa tamasha la kimataifa kwa ushirikiano na #Utawala wa Uganda wa kidikteta, @MTVBaseAfrica

“Sio tu kwamba litakuwa linafuta uhalifu uliofanywa na utawala huo, lakini pia litaathiri wasanii wote walioteuliwa,” Jeffrey Smith aliandika ujumbe huo.

Tamasha hilo maarufu kama MAMAs, ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika Kampala, lilikuwa litaendeshwa kwa njia ya moja kwa moja mtandaoni kwasababu ya janga la virusi vya corona.

Pia ingekuwa ni mara ya kwanza tuzo hizo zinatolewa nchini Uganda.

Tuzo hizo ambazo mara ya kwanza zilifanyika 2008 mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini mwaka 2016, mwaka 2009 zilifanyika nchini Kenya iliyopo Afrika Mashariki jijini Nairobi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad