Kuelekea kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho baina ya Simba SC na African Lyon, Afisa Habari wa Mabingwa hao wa Nchi, Haji Manara amedai kuwa malengo yao Makuu ni kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu na FA, huku akiongea kwa msisitizo kuwa ni bora watolewe hatua ya ‘group stage’ ya CAF Champions League lakini ni lazima kuubeba Ubingwa wa Ligi Kuu.
Manara amesema kuwa kwa Simba Ubingwa wa Ligi Kuu ni ‘Do Or Die’ ”Tuna shida moja Simba SC, sijui imetokea wapi, ipo kwa miaka mingi tangu mimi mdogo, ukimaliza kucheza na timu kubwa ukashinda, unapokwenda kucheza mechi ya kawaida mara nyingi hatufanyi vizuri, kwa hiyo nilimkubusha mwalimu Matola awakumbushe wachezaji na wewe na kocha wako Mkuu, tunakwenda kucheza mechi na African Lyon FC tushatolewa na Green Worriors, tushatolewa na Mashujaa timu za daraja la kwanza tusichukulie powa.”
”Nikamwambia kufungwa na African Lyon FC ni mbaya zaidi kuliko tungefungwa na Al Ahly, kufungwa hata kwa penati na African Lyon ni dhambi kubwa ambayo hata wana Simba hawataki kuisikia.”
”Mwalimu wetu tumemkumbusha Simba hii ni bora tutolewe kwenye ‘group stage’ lakini lazima tuchukue Ubingwa wa Ligi Kuu na FA. Ni afadhali tutolewe kwenye ‘group stage’ kwetu sisi Ubingwa wa Ligi Kuu ni ‘Do Or Die’.
”Malengo ya Simba, kuna malengo makuu na malengo mama, malengo makuu ya Simba ni Ubingwa wa Ligi Kuu na Ubingwa wa FA, lengo mama ni kufika hatua ya Nusu Fainali ya CAF Champions League.”
Simba SC kesho itakutana na African Lyon kwenye michuano hiyo ya kombe la Shirikisho mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkapa.