Uganda intaneti imerudi upya, tumieni Intaneti sasa




Serikali ya Uganda imetangaza kuondoa vizuizi vyote ilivyokuwa imeviweka katika intaneti na mitandao ya kijamii.  “Tuaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza, lakini ilikuwa ni kwa ajili ya usalama wa taifa letu,” Peter Ogwang, Waziri wa mawasiliano, aliandika kwenye tweeter.



Aliongeza: “Tuwe wateja wa kujenga na sio kubomoa , tuwe wateja wazuri wa mitandao ya kijamii.”

Huduma ya mitandao ya kijamii ilizuiwa usiku wa kuamkia tarehe 14 Januari, siku ya uchaguzi mkuu.

Rais Yoweri Museveni alishutumu kampeni za mitandao ya kijamii kuwa na ubaguzi.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Facebook kusema kuwa inazifungia zaidi ya akaunti 200 zinazohusiana na kampeni za chama tawala.

Kampuni ya mitandao ya kijamii ilidai kuwa akaunti hizo zilikuwa zinasambaza taarifa zisizo sahihi kudhibiti mijadala kabla ya siku ya kupiga kura.

Facebook ilisema akaunti hizo zilikuwa za Uganda, na zilikuwa zinatuma taarifa gushi kwa wananchi wake na hata kutuma taarifa hizo mara kadhaa ili kuzipa taarifa hizo umaarufu zaidi.

Mkuu wa taarifa za vitisho Facebook, David Agranovich, alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa unahusisha akaunti feki zilizohusisha moja kwa moja wizara ya mawasiliano na teknolojia.

Facebook pia iliondoa akaunti 139 za Instagram.

Akaunti hizo zilikuwa zilikuwa zinamuunga mkono Rais Museveni na chama chake cha National Resistance Movement.

Mpinzani wake mkuu ambaye ni mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa Robert Kyagulanyi anayefahamika kama Bobi Wine, alikuwa na miaka minne tu wakati wakati Bw. Museveni aingie madarakani mwaka 1986.

Bwana Museveni ameingia muhula wa sita wa utawala wake baada ya kuchuana vikali na mpinzani wake Bobi Wine, ambaye anadai matokeo yalikuwa ya uongo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad