Serikali imeweka wazi chanzo cha kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, na kusema kuwa amefariki kutokana na maradhi ya moyo na aliugua kwa muda mfupi.
Akisoma wasifu wa Marehemu Balozi Kijazi, Katibu Mkuu Utumishi Laurean Ndumbaro, amesema kuwa Balozi Kijazi, alizaliwa mkoani Mwanza akiwa ni mtoto wa pili kwenye familia ya watoto 10.
“Balozi Mhandisi John Kijazi ameugua kwa muda mfupi ambapo Februari 1 , 2021, alilazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, hadi mauti yalipomfika na amefariki kwa maradhi ya moyo akiwa na miaka 60”, amesema Dkt. Ndumbaro.
Marehemu Balozi Mhandisi John Kijazi ameacha mke, watoto watatu pamoja na wajukuu wawili, na atazikwa leo Februari 20, 2021, wilayani Korogwe mkoani Tanga.