Unaambiwa Mpaka sasa Tanzania Magari Yanayotumia Gesi Yafikia 400

 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Serikali ya Mdhibiti wa Mkondo wa juu wa Petroli (PURA) Charles Sangweni ambae ni Mhanidisi wa Petroli pia, amesema hadi sasa Nchini Tanzania kuna magari zaidi ya 400 yanayotumia mfumo wa gesi kujiendesha.


Amesema katika magari hayo 400 yapo pia magari ya Kiwanda cha cement cha Dangote Mtwara ambapo magari yao yote karibu 70% yameshabadilishwa yanatumia gesi sasa hivi na ukipishana nayo ukiyaangalia nyuma ya kichwa kuna matenki kama manne yamepangwa, ile ni gesi.


“Shughuli zetu zilianza rasmi mwaka 2015 baada ya sheria ya Petroli kuanzishwa na tumejikita sana kusimamia shughuli za utafutaji, uzalishaji na uendelezaji wa mafuta Nchini na hadi sasa tumegundua gesi asilia kiasi cha futi za ujazo Trilioni 57.54 na bado tafiti zinaendelea” —— Sangweni.


Unataka kufahamu ukitumia gesi unaokoa shilingi ngapi ambazo ungezitumia kwenye mafuta au petroli? post yenye ufafanuzi itafata hapahapa kwa millardayo. #MillardAyoAMAZING

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad