Video Ikionesha Wanafunzi Wakikimbia Kipimo Kipya cha Corona, Nigeria Yakanusha



Video inayosambaa mtandaoni ikiwa inaonesha madai ya uongo ya watoto wa shule wakiwa wanakimbia kuchomwa chanjo ya corona kwa lazima.


Ukweli ni kwamba video hiyo ilipigwa miezi saba kabla ya hata kisa cha kwanza cha mgonjwa wa corona kuripotiwa nchini China na kabla hata ya chanjo yeyote ya corona kuanza kutengenezwa.

Video hiyo inaonesha watoto wakikimbia kwenye korido huku wengine wakiruka kutoka kwenye madarasa na wengine wakikimbia na mabegi yao.

Mtumiaji mmoja wa Facebook alisema watoto hao walikuwa wanakimbia kuchomwa chanjo ya corona.


Lakini video hii ilitumika na TV ya Nigeria, Daily Trust tarehe 26 Mei, 2019, ilisema kulikuwa na mlipuko wa mabomu ya kutoa machozi katika shule ya sekondari ya Community iliyopo Port Harcourt, kusini mwa Nigeria.

Kituo cha TV cha Abuja-kinasema kijana mmoja mwenye miaka 17-alikuwa amebeba mikebe ya mabomu ya gesi na kuwaonesha wanafunzi wenzake.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad