Vifo 500,000 vya corona Marekani Vinaumiza sana'- Biden




Rais wa Marekani, Joe Biden amehutubia taifa baada ya kurekodi vifo 500,000 vilivyotokana na virusi vya corona, idadi kubwa zaidi kufikiwa ulimwenguni.
''Kama taifa, hatuwezi kukubali mwisho huu mbaya. Tunapaswa kuepuka kufa ganzi kwa huzuni,'' alisema.

Rais na Makamu wa Rais , na wake zao, kisha walikaa kimya nje ya White House wakati wa tukio la kuwasha mshumaa.

Zaidi ya Wamarekani milioni 28.1 wamepata maambukizi ambayo pia ni idadi ya juu zaidi duniani.

''Leo ninawaomba Wamarekani kukumbuka. Kukumbuka wale tuliowapoteza na kuwakumbuka tuliowaacha,''

Rais Biden alisema akiwataka Wamarekani kupambana na Covid-19 kwa pamoja.

Bwana Biden aliamuru bendera zote kwenye maeneo ya serikali zishushwe nusu mlingoti kwa siku tano.

Katika ikulu ya White House, alifungua hotuba yake kwa kueleza kuwa idadi ya Wamarekani waliokufa na virusi vya corona ni kubwa zaidi kuliko ilivyokuwa idadi ya vifo vya vita vya kwanza vya dunia, vita vya pili vya dunia , na vita vya Vietnam ukijumuisha kwa pamoja.

"Leo tunaashiria hatua mbaya sana, yenye kuumiza moyo - 500,071 wamekufa," alisema.

"Mara nyingi tunasikia watu wakielezewa kama Wamarekani wa kawaida," aliendelea kusema. "Hakuna kitu kama hicho, hakuna kitu cha kawaida juu yao. Watu tuliopoteza walikuwa zaidi ya watu wa kawaida . Walikuza vizazi. Walizaliwa Marekani, walihamia Marekani."

"Wengi wao walivuta pumzi yao ya mwisho wakiwa peke yao Marekani," aliendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad