Wafanyakazi 27 wa rais wa Sudan Kusini wana Corona



Wafanyakazi ishirini saba wa ofisi ya rais wa Sudan Kusini wamepatwa na virusi vya Covid-19, Wale walioathiriwa zaidi ni wafanyakazi wangazi ya chini na wafanyakazi walinda usalama wa rais.



Rais Salva Kiir hajapatikana na virusi, kulingana na msemaji wake Ateny Wek Ateny.

“Ni kweli, zaidi ya wafanyakazi 20 wamepatikana na virusi, hasa wale wa kitengo cha ulinzi na wafanyakazi wa ngazi ya chini katika ofisi ya rais.

“Mimi ni mmoja wa maafisa wawili wa ngazi ya juu walipatikana na corona, mimi na mchanganuzi wa sera – idadi jumla ni 27,” Bw Ateny aliiambia BBC.

Amesema kuwa wananyakazi wote wa Ikulu ya rais katika mji mku Juba watapima tena kwa awamu ya pili kama tahadhari. Mawaziri wawili na mshauri wa rais pia walipimwa mara ya pili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad