Waliohusika na zabuni zinazohusu covid-19 Afrika Kusini kukiona



Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema atachukua hatua ''kali'' na ''stahiki'' dhidi ya wazabuni wanaohusiana na virusi vya corona.

Bw. Ramaphosa amesema mashirika ya serikali yameelekezwa kutolipa watoa huduma kusubiri matokeo ya uchunguzi au hatua ya mahakama.


"Hawatafurahia faida yao iliyopatikana kwa namna ovu, kwani hatua zimechukuliwa kupata pesa zilizoibiwa, pamoja na kufungia akaunti za benki," alisema.


Ripoti ilitolewa mwaka jana kuhusu matumizi ya fedha za kupambana na Covid-19, ilibaini gharama kubwa na udanganyifu.


Vifaa vya kujikinga (PPE) zilinunuliwa kwa bei mara tano zaidi ya gharama ambayo hazina ya nchi hiyo imeelekeza


Rais Ramaphosa amesema '' wamepata funzo kubwa'' kutoka kwa watu ambao ''wametumia mwanya wa uharaka iliyopo''.


"Uzoefu wa taifa letu katika ununuzi wa vifaa na huduma muhimu wakati wa janga la kitaifa ni suala la aibu ambalo linapswa likomeshwe kwa nguvu,'' Alisema.


Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Cyril Ramaphosa, Pole kwa kuzungukwa na Walafi na Wabadhirifu.
    Do you know.? in such case, What will Mmagufuli Do..!!?? he will Magulify.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad