Waliomteka mfanyabiashara, kuomba rushwa wakiri mashtaka

 



Arusha. Waliokuwa askari  wa Jeshi la Polisi na wenzao watano wanaokabiliwa na mashtaka ya kumteka mfanyabiashara wa madini,  Sammy Mollel na kumuomba rushwa ya Sh30 milioni wameandika  barua za  kukiri mashtaka sita.


Mashtaka waliyokiri ni ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha haramu na kupanga njama za kujipatia fedha kinyume na utaratibu ambapo  awali walishachukua Sh10 milioni kati ya milioni 30 walizohitaji kutoka kwa  Mollel.


Wakili upande wa utetezi Charles Kagirwa amesema wateja wake wameshaandika barua ya kukiri mashtaka hayo.


Kesi hiyo namba 3 ya mwaka  2021 leo Jumatano Februari 20,2021 imesikiliwa na hakimu mkazi mfawidhi, Rose Ngoka ambaye alisema hajaridhishwa na barua yao ya kukiri mashtaka sita na kuahirisha kesi hiyo hadi Februari 24, 2021 itakapotajwa tena.


Kabla ya kupandishwa kizimbani, askari hao walishtakiwa kijeshi na walibainika na tuhuma na kufukuzwa kazi kwa kosa la kupokea  rushwa ambao ni Heavenlight Mushi aliyekuwa kitengo cha Intelijensia Mkoa wa kipolisi Kinondoni jijini Dar es Salaam, Gasper Paul kitengo cha Intelijensia makao makuu Dodoma na Bryton Murumbe.


Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Joseph Chacha, Leonila Joseph, ,Nelson Lyimo na Omary Alphonce.


Washtakiwa wote wamerudishwa katika gereza la Kisongo kwa kuwa mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.


Polisi walivyomteka mfanyabiashara, kuomba Sh30 mil

Imeandikwa na Amina Ngahewa pamoja na  Husna Issa, mwananchi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad