Na Amiri Kilagalila,Njombe
Baadhi ya wamiliki wa vyombo vya moto hususani bajaji na pikipiki(BODABODA) wametajwa kuwa ndiyo sababu ya kutokea kwa ajali za barabarani kutokana na kuwakabidhi vyombo vya usafari madereva ambao hawana leseni na vyeti ambavyo vinaonyesha wamepata mafunzo ya usalama barabarani.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani kutoka jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako MORIS KASINISALA wakati akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa kitendo cha wamiliki wa vyombo vya moto kuwakabidhi madereva ambao hawana leseni na wale ambao hawana vyeti ndiyo sababu ya kuongezeka kwa ajali za barabarani kwa kuwa hawajui sheria na taratibu na usalama barabarani.
Aidha amesema wamiliki wa vyombo vya moto kuwakabidhi madereva vyombo hivyo bila kuwa na vyeti vya mafunzo na leseni ni kosa kisheria na wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
“Wamiliki wa vyombo hakikisheni kwanza dereva unayempatia chombo chako iwe ni bajaji au piki piki kuwa anayo leseni halali inayomtaka aendeshe chombo hicho,hawa wamiriki huwa wanawakabidhi vyombo kwa madereva bila kuangalia huyu mtu ana leseni:”alisema Moris Kasinisala
Baadhi ya madereva bajaji na bodaboda ambao wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani mjini Makambako wamesema ili kupunnguza ajali za barabarani ni lazima wamiliki wa vyombo vya moto nao wapewe elimu ya namna ya kutunza vyombo vyao na siyo kujali maslahi pekee.
“Kuna watu utakuta wanakuwa wanafanya ujanja wanaonyesha leseni bila vyetu kwa kuwa hawana mafunzo,nawaasa mabosi wanapomkabidhi chombo dereva wawe wanamkagua kabla hajaingia barabarani,kwasababu vijana wanaendesha kwa mazoe na ajali zinatokea mara kwa mara”walisema madereva
Hata hivyo mratibu wa sheria na kanuni za usalama barabarani wa chuo cha New vision VTC driving schools Njombe PATRICK MWENGU amesema elimu kwa madereva wa vyombo vya moto na wamiliki ndiyo itakayo saidia kuondoa kabisa ajali ambazo zinatokea barabarani.
“Mtu akishapita shuleni anakuwa na weledi kuhusu kila kitu kilichopo bara barani na anajua hapa pana nini kwenye zebra nifanyanje hii itapunguza ajali”alisema Patrick Msemwa