Wanafunzi washindwa kwenda shule kuhofia kuawa na tembo

 


Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro wameiomba Wizara ya Maliasili na Utalii  kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA), kuyadhibiti makundi ya tembo kutoka hifadhi ya Taifa ya Tsavo ambayo yamevamia makazi ya watu na kuharibu mazao.

Diwani wa Kata ya Kwakoa, Kiende Mvungi, akizungumza Jana katika mkutano wa Baraza la Halmashauri ambalo llijadili taarifa za Utekelezaji wa shughuli za Maendeleo katika kata kwa kipindi cha Robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2020/2021 amesema wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Kwakoa, wameshindwa kwenda shule kutokana na makundi ya tembo kutoka hifadhi ya Taifa Tsavo nchini Kenya.


"Wanafunzi wa wanaosoma katika shule ya Msingi Kwakoa wameshindwa kwenda shule kutokana na kuhofia kuawa na makundi haya ya tembo," amesema Mvungi.


Naye Diwani wa Jipe, Dk. Ally Kidaya, amesema suala la tembo limekuwa Ni tatizo kubwa kwa wananchi wa Kata ya Jipe, jambo ambalo limechangia baadhi ya wananchi hao kulazimika kuyakimbia makazi yao.


"Tembo hawa wanavuka kutoka Kenya kuja kuharibu mazao kwa kiwango kikubwa, wananchi wa maeneo haya wamekuwa wakilazimika kuyakimbia makazi yao," amesema.


Akichangia hoja hiyo Diwani wa Kata ya Toloha, Palesio Makange, amesema makundi hayo ya tembo yamekuwa tishio kubwa kwa wananchi kutokana na kuvamia mazao ya wananchi na kusababisha uharibifu mkubwa na kuziomba Mamlaka husika kuangali namna ya kuwadhibiti ili wananchi waendelee kuishi kwa amani.


"Wako baadhi ya wananchi wamedhurika kutokana na wanyama hawa hivyo tunaiomba


serikali iangalie namna ya kuwafidia wananchi hawa," amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad