Dodoma. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema chama kimeanza kufanya tathmini ya uchaguzi mkuu 2020 ili kuwabaini wale wote waliokisaliti kwenye uchaguzi huo.
Dk Bashiru alieleza hayo jijini hapa jana, katika ofisi za makao makuu ya chama hicho wakati wa mdahalo wa maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwake.
Alisema baada ya kufanya tathmini hiyo watakaobainika kukisaliti chama hicho kwa kuhongwa, kutumia madaraka yao vibaya hawataachwa salama na kwamba, watawajibishwa kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Mwananchi