Watu 150 hawajulikani walipo baada ya pande la barafu kuanguka India





Watu 9 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 150 hawajulikani walipo baada ya pande kubwa la barafu katika safu ya milima ya Himalaya kuanguka ndani ya mto katika jimbo la Uttarakhand kaskazini mwa India siku ya Jumapili.

 Ajali hiyo imesababisha mafuriko, kuvunjika kwa mabwawa huku barabara na madaraja yakisombwa. Wafanyakazi wa mabwawa mawili ya kuzalisha umeme wanahofiwa kusombwa na mafuriko pamoja na wanakijiji wengine waliokuwa karibu na mto. 

Vidio zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha jinsi pande la barafu lilivyoanguka na kuachia maji yaliyosababisha tafrani kubwa.

 Jimbo la Uttarakhand lililoko kwenye safu ya milima ya Himalaya limekuwa likikabiliwa na mvua kubwa. Waziri mkuu wa India Narendra Modi ametoa pole na kutangaza fidia ya kifedha kwa walioathiriwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad