Wanachama 6 wa kikundi cha upande wa kulia nchini Marekani wameshtakiwa kwa kupanga uvamizi kwenye jengo la Bunge.
Kulingana na taarifa ya Wizara ya Sheria, wanachama wa kikundi cha Oath Keepers ambao ni Graydon Young, Kelly Meggs, Connie Meggs, Laura Steele, Sandra Parker na Bennie Parker, walituhumiwa kwa kupanga njama ya kutekeleza uvamizi kwenye jengo la Bunge mnamo Januari 6.
Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa wanachama hao 6 wanaohusika walifanya njama dhidi ya kuvamia na kupora mali za serikali ya Marekani na kuingia kwenye majengo ya umma kinyume cha sheria.
Taarifa hiyo pia ilisema kuwa wanachama 5 isipokuwa Bennie Parker waliingia katika jenge la Bunge kwa kuvalia kitofauti na kutembea kwa utaratibu wa kijeshi, ambapo baadaye wote 6 walishirikiana na watu wengine 3 ambao walituhumiwa kwa kuvamia jengo la Bunge mwezi uliopita.
Hapo awali, Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) ilitangaza mwezi uliopita kwamba mkuu wa "Oath Keepers" Thomas Edward Caldwell mwenye umri wa miaka 65, Jessica Watkins na Donovan Ray Crowl walikuwa wakipanga uvamizi kwenye jengo la Bunge mnamo Januari 6.