Waziri Mkuu atoa neno uvaaji wa barakoa

  


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka Watanzania kuvaa barakoa wanazotengeneza wenyewe au zile zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini na siyo kuvaa zinazozalishwa nje bila kujiridhisha mahali zinapotoka.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 20, 2021, mkoani Tanga, mara baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ambaye amezikwa leo nyumbani kwake Korogwe, ambapo pia amesisitiza suala la wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kwamba serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa magonjwa ya mlipuko yaliyopo kwa sasa.


"Nimeona leo tabia ambayo tuliizungumza hata mwaka jana watu wawe na tabia ya kunawa, wananawa, kutumia vitakasa mikono watu wanafanya na wengine pia wamevaa barakoa, barakoa utaivaa pale ambapo unajua shughuli zako za siku hiyo zitakupelekea kupata huduma au kutoa huduma na mwingine hakuna aliyekataza muhimu kila mtu aende kwa tahadhari", amesema Waziri Mkuu


"Barakoa hizi ni bora tukajiridhisha zinatoka wapi, bora ukatengeneza ya kwako au iliyotengenezwa hapa nchini Tanzania, barakoa ni kinguo tu kinachozuia hayo mate yasie yakatoka au ukapokea vitu vingine hili jambo ni muhimu sana tulizingatie", amesisitiza Waziri Mkuu

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad