WHO yaunga Mkono Chanjo ya Oxford isiyozuia Aina Mpya za Corona

 

Shirika la afya dunaini limeshauri matumizi ya chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford na AstraZeneca hata kama nchi zinakabiliana na aina mpya za virusi vya corona.

Baadhi ya aina za virusi hivyo zinaonekana kuifanya aina hiyo ya chanjo kutokuwa na ufanisi wa kutosha wa kuzuia maambukizi.


WHO pia inasema chanjo hiyo inaweza kutumiwa kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65, jambo linalozuiwa na baadhi ya nchi.


Kutenganisha muda wa utoaji wa dozi za chanjo hiyo, kama inavyofanyika nchini Uingereza, kunaifanya chanjo hiyo kuwa na ufanisi zaidi, inashauri WHO.


Chanjo ya Oxford vinaonekana kama "chanjo ya dunia " kuutokana na kwamba ni nafuu, inaweza kutengenezwa kwa wingi , na inaweza kutunzwa katika friji ya kawaida.


Hatahivyo, imeibua utata juu ya ufanisi wake, wengi wakijiuzliza iwapo inapaswa kutumiwa miongoni mwa wazee na ni kwa muda gani dozi mbili zinapaswa kutulewa, kutokana na ukosefu wa taarifa(data) kuhusiana na hilo.


Kikundi cha wataalamu na washauri wa mkakati wa utoaji chanjo wa cha WHO, kinachofahamika kama Sage, kimekuwa kikichunguza kwa kina ushahidi kutoka katika majaribio ya chanjo.


Ushauri wake kwa sasa unasema chanjo ya Oxford ina una ufanisi kwa 63%.


Hata hivyo data za awali kutoka nchini Afrika Kusini zilionesha kuwa chanjo hiyo inayoa''kinga kidogo " dhidi ya ugonjwa vijana wanaougua kwa kiwango cha chini na cha kadri.


Mkurugenzi wa WHO wa masuala ya utaji wa chanjo, Dkt Katherine O'Brien, alisema kuwa utafiti wa Afrika Kusini "haukukamilia" na ulikuwa ni "ubashiri " chanjo bado inaweza kuzuwia mtu kuugua sana.


Aina mpya ya virusi nchini humo imegeuka na kupata umbo jipya ambayo inaonekana kusaidia kuondoa kinga ya chanjo na ile mtu anayoipata baada ya maambukizi ya awali.


Hatahivyo wanasayansi wa Oxford sbado wanatarajia chanjo yao inaweza kuzuia watu kuugua sana kutokana na Covid-19 na kuhitaji matibabu ya hospitali.


" Hakuna sababu ya kutowasahauri watu kuitumia hata katika nchi ambazo zina aina mpya za corona zinazozunguka ," alisema Dkt Alejandro Cravioto, mwenyekiti wa wataalamu na washauri wa mkakati wa utoaji chanjo wa cha WHO.


Kumekua na ukosoaj juu ya ukosefu wa data kuhusu ufanisi wa chanjo miongoni mwa wazee huku baadhi ya nchi , ikiwani pamoja na Ufaransa na Ujerumani, zikishauri dhidi ya matumizi yake kwa watu wenye mri wa zaidi ya miaka 65.


WHO ilisema kuwa ingawa kulikuwa na idadi ndogo ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 walioshiriki majaribio ya chanjo hiyo, tafiti nyingine zinaonesha kuwa watu wenye umri mkubwa walikuwa na kinaga ya mwili karibu sawa na ya vijana watu wazima majaribio kwahiyo chanjo inapaswa kutumiwa kwa wote.


Washauri wa kisayansi pia walisema kutoa dozi mbili, ya kwana na nyingine baada ya wiki nane kunaongeza ufanisi wa chanjo na kutoa kinga kubwa dhidi ya kuugua.


mwanzoni, WHO ilikuwa imeshauri kuwe na muda wa wiki sita baina ya chanjo ya dozi ya kwanza na ya pili, isipokuwa kwa hali za kipekee za nadra.


Prof Sarah Gilbert, mchunguzi mkuu wa jaribio la chanjo ya Oxford alisema: "Ni taarifa nzuri sana kwamba WHO imeshauri matumizi ya chanjo ya Sars CoV-2 ya kwanza kutengenezwa katika Oxford.


"Uamuzi huo ulitoa fursa ya kusambazwa kwa matumizi ya chanjo hiyo kwa ajili ya kuwalinda watu dhidi ya Covid-19 na pia kudhibiti janga la corona .";


 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad