ACT Magufuli aacha pigo kwa Taifa




CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesema kifo cha aliyekuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni Pigo kubwa katika taifa na kuwataka Watanzania wote kuwa wavumilivu kipindi choote cha msia


Kauli hiyo ilitolewa na Makamo Mwenyekiti wa chama hicho Juma Duni Haji akiwa katika Afisi Kuu ya CCM iliyopo Kiswandui Zanzibar kwa ajili ya kutoa mkono wa Pole kwa viongozi wa CCM na Viongozi wake.



Alisema kuondokewa na mwenyekiti na akiwa Rais ni jambo zitoo sana na kusema inahitajika uwepo wa subra miongoni mwa Watanzania na familia na wanaCCM.



Alisema kuwa Rais John Joseph Pombe Maguful alikuwa Rais alyesimama katika majukwaa na kusema wazi wazi kuwa anayaunga mkono na ataendeleza Maridhiano.



“Sasa ni wajibu wetu sisi uliohai kyaendeeza na kuyaenzi ili walioazisha ambao washatangulia mbele ya haki tuwatendee haki” alisema Haji



Duni alisema Viongozi wa CCM jinsi walivyowapokea  ni kiasi gani  kuonesha kua yale maridhiao yaliosisiwa na  Malim Seif  pamoja na baadhi vingozi wa CCM yanaenendelezwa na kutekelezwa kwa vitendo.



Alisema kuwa Viongozi wa chama cha Mapinduzi alipofariki aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT wazalendo walifika AFisini kwao Vuga kutoa mno wa Pole.



“Kwa hali hiyo uaona ni kiasi gani maridhiano yanaendelezwa na tumeaambiana kuwa Wazanzibar na watanzania Kwa jumla sisi ni wamoja tuendeleze umoja wetu” alisema Duni.



Alisema kuwa  ama raiya wamefiliwa na rais wao wanatoa pole kwa niaba ya chama cha ACT Wazalendo kwa mama Samia Suluhu Hassan  pamoja na kutoa  polea kwa wanachama wote wa CCM kuondokewa na mwenyekiti wao ambapo  ni pigo kubwa kwa Taifa.



Duni Haji alieleza kuwa  Wazanzibar ni wamoja na hapana budi kushirikiana hasa katika matukio haya ya misiba ambayo yameshawahi kutokea.



Hata hivyo alisema matukio kama hayo huwa sababu nyengine ya kuwaunganisha wazanzibar na kuweka pembeni tofauti zao za kisiasa  na huungana pamja kata kujega tafa.



“Hakuna mtu aliyetegemea kama matukio hayo ya kifo yatatokea akini ni kazi ya mumba haina makosa”  alisema haji.



Kwa upande mwengine Duni alisema kuwa marais waliopo sasa wote ni wapya na wanategemea kuwa na siasa za umoja n mashiriiano kwa maslahi mapana ya taifa.



“Tunampongeza mama Samia kwa kuchukuwa dhamana kubwa na tunategemea kuwa na siasa za marihiano katika ardhi ya Tanzania” alisema



Sambamba na hilo aliwataka watanzania kushirikiana pamoja katika kusitiri kiongozi huyo ambaye alifariki tarehe 17/3/2021.



Mapema Asubuhi uongozi wa ACT wazalendo ukiongozwa na Makamo huyo walifika Wizara ya Habari Zanzibar na kuweka saini zao katika kitabu cha Maombolezo.



Wakati huo huo waliwaomba wananchi wooe wahudhurie katika kuuwaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati John Joseph Pombe Magufuli wakiwawamevaa Barakaowa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad