Ajali ya ndege yatokea nchini Kazakhstan

Watu 4 wameripotiwa kufariki katika ajali ya ndege aina ya AN-26 ilianguka wakati wa kutua nchini Kazakhstan.

Kulingana na taarifa ya habari ya huduma ya uwanja wa ndege wa Almaty, ndege aina ya AN-26 inayomilikiwa na Kamati ya Usalama ya Kitaifa ya Kazakhstan, ilianguka karibu na kijiji cha Kızıltu nchini Kazakhstan wakati wa kutua.

Ilitangazwa kuwa ndege hiyo iliyofanya ajali ilikuwa ikiruka kwa ajili ya msafara wa Nur-Sultan kuelekea Almaty.

Ndege iliyokuwa ikiruka kutoka mji mkuu Nur-Sultan kwenda Almaty, ilianguka kabla ya kufikia barabara ya kutua.

Safari ya ndege hiyo ilikatishwa mwendo wa saa 17:20 za jioni na ishara ya dharura ikatolewa.

Moto uliotokea baada ya ndege kuanguka ulizimwa.

Katika ndege hiyo iliyokuwa na wanajeshi 6, watu 4 walifariki na wengine 2 walijeruhiwa na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Safari za ndege zilicheleweshwa katika Uwanja wa Ndege wa Almaty kutokana na ajali hiyo.

Timu za utaftaji na uokoaji zinaendelea na shughuli katika eneo la tukio.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad