Na Timothy Itembe Mara.
FAMILIA ya marehemu Bibi,Hilda Nyamahiri (61) katika kipindi hiki cha maombolezo ya kitaifa cha kufiwa na Rais John Pombe Magufuli imepongeza mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Tarime kwa jitihada za kuhakikisha mwili wa mpendwa wao unapatikana na kuzikwa kwa heshima za marehemu.
Akoingea na mwaandishi wa habari hizi kijana wake mkubwa,Jeremia Marwa alitumia nafasi hiyo kupongeza mkuu wa wilaya,Mtemi Msafiri pamoja na Jeshi la Polisi kuhakikisha mwili wa mamayao mpendwa unapatikana baada ya kutekwa na majambazi akiwa nyumbani kwake usiku saa 2 Mach,13,2021 akiwa anapika.
“Mama alitekwa na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi majira ya saa 2 usiku akiwa nyumbani kwake akipika chakula ambapo alipiga yoe midomi miwili tu ili kuomba masaada lakini jitihada hizo ziligonga mwamba asubuhi majirani walifika kuona kilichijiri katika nyumba hiyo ambapo walifika na kukuta damu imetapakaa chumbani na mama hayupo jitihada za kumtafuta zikaanza”alisema Marwa.
Marwa aliongeza kuwa majirani wakiambatana na jeshi la polisi chini ya mkuu wa wilaya,Mtemi Msafiri walitafuta kila kona lakini baada ya siku taklibabani 8 walifanikiwa kukuta mwili wa marehemu kijiji cha Ng’aramwa karibu na kijiji cha Nyarutu ukiwa umekatwa katwa vipande na kusondekwa ndani ya mfuko wa kupakia mahindi na kutupwa ndani ya shimo.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Kebikiri,Juma Gidion alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo mgogoro wa Ardhi ulisababisha mama huyo kutolewa uhai kwake na mahasimu wake.
Mwenyekiti huyo alimaliza kwa kusema kuwa mazishi ya Hilda hapo jana yalichukua sura mpya ambapo wananzengo walibomoa nyumba zilizokuwa ndani ya uwanja wa marehemu baada ya kukuta wenyeji wamekimbia miji yao ambao ndio wanashukiwa kutenda tukio hilo la kinyama.
Mussa Magesa ambaye ni kijana wa marehemu alibainisha kuwa inadaiwa watekaji wa mama huyo ni pamoja na Mhoni Nyahucho,Albinus Nyahucho na Mwita Nyahucho ambao walikuwa wanashitakiana katika Baraza la Ardhi na nyumba la wilaya Tarime ambapo marehemu aliwashinda na kesi kuamriwa washitakiwa kupisha eneo hilo kabla ya tarehe 17 machi,2021.
Mgesa aliongeza kusema kabla ya kuhama wadaiwa hao walikuja kufanya utekeji wa kihasimu na kufanya mauaji ya kikatili kwa mama huyo ambapo walimkata kata vipande vipande na kumfunga ndani ya mfuko wa mahindi na kwenda kumtupa ndani ya shimo umbali wa kilo mita zaidi ya 30 kutoka mtaani kwake Kebikiri .
Familia hiyo wameiomba serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama ili kutumia nguvu za iada kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa licha ya kuwa mtuhumiwa mmoja amekamatwa na yuko mahabusu ili kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.