Biden ampa Harris jukumu la kushughulikia changamoto ya uhamiaji mpakani




Rais Joe Biden wa Marekani amempa jukumu makamu wake Kamala Harris la kuongoza juhudi za Ikulu ya White House za kukabiliana na changamoto ya uhamiaji katika mpaka wa kusini mwa taifa hilo, na kushirikiana na mataifa ya Amerika ya Kati kushughulikia chanzo cha tatizo hilo.
Biden ametoa tangazo hilo wakati yeye na Harris walipokutana White House jana Jumatano, pamoja na waziri wa afya na huduma za kibinaadamu, Xavier Becerra, waziri wa usalama wa ndani, Alejandra Mayorkas, na washauri wengine wa uhamiaji kujadili ongezeko la wahamiaji, ikiwa ni pamoja na watoto wasio na wazazi ambao wamefika kwenye mpaka huo katika siku za karibuni.

Biden, ambaye amekosolewa vikali na Republican kuhusiana na ongezeko hilo, ana matumaini ya kuwaonesha Wamarekani kwamba analichukulia suala hilo kwa umakini mkubwa, akilenga kuzuia mzozo mkubwa wa kibinaadamu na kisiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad