Bobi Wine na Hofu ya Kumiliki Gari la Kifahari




KIONGOZI wa upinzani wa Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine amejikuta akiwa katika hofu kubwa kwa madai ya kuwa na gari la kifahari ambalo haliingii risasi, kulingana na taarifa katika gazeti la Daily Monitor.

 

 

Gari hilo limevutia mamlaka nchini Uganda, huku mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru ya Uganda (URA) ikisema maelezo yaliyotolewa si sahihi na kwamba thamani yake iko chini kuliko inavyostahili kuwa. URA, sasa inataka gari hilo kukaguliwa upya.

 

 

Bobi Wine, hata hivyo amekataa kuwasilisha gari hilo kwa misingi kwamba agizo hilo haliambatani na sheria, kulingana na taarifa yake iliyonukuliwa na gazeti la Daily Monitor.

 

 

“Japo mna uwezo chini ya kifungu cha 236(d) cha usimamizi wa forodhani katika Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, kukagua bidhaa, hamna uwezo wa moja kwa moja kukagua tena bidhaa ambayo ilikuwa katika (bohari lenu), na ambayo ilikuwa imekaguliwa, kutathmini kodi na kodi hiyo kulipwa kabla ya bidhaa kutolewa kwa mmiliki/mlipa kodi,” ilisema.

 

 

Gari hilo liliingizwa nchini na kusajiliwa Kenya mwaka jana na kisha kupelekwa Uganda kupitia mpaka wa Busia. Katika ujumbe alioweka mtandaoni Februari 21, Bw. Kyagulanyi alidai kuwa gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lilitolewa kwake kama msaada na marafiki na wafuasi wake nchini Uganda na ughaibuni:


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad