Brazil imethibitisha vifo vilivyotokana na maradhi ya COVID-19 kupindukia 300,000 hadi jana Jumatano na kulifanya taifa hilo kuwa la pili kufikia idadi hiyo, huku maambukizi yakiongezeka na kushuhudiwa ripoti za idadi kubwa ya kila siku ya vifo katika siku za karibuni.
Marekani ilifikia idadi kama hiyo Disemba 14 mwaka jana, lakini ina idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na Brazil.
Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, idadi hii ya sasa huenda ikawa imechangiwa na mabadiliko yaliyofanywa na serikali katika mahesabu.
Waziri mpya wa afya Marcelo Queironga aliwaambia waandishi wa habari kwamba angerejelea idadi hiyo ili kuhakikisha kama haikupunguzwa.
Magavana na mameya wa majimbo wameeleza wasiwasi wao kwamba mwezi ujao wa Aprili huenda ukawa mbaya zaidi hasa kwa hospitali za nchini humo ambazo tayari zimeelewa.