Msanii wa kike wa BongoFleva Malaika amesema wakati anaanza muziki alikutana na changamoto ambayo ilimfanya kumaliza mwaka mzima bila ya kufanya mazungumzo na baba yake ambaye alikuwa anaamini muziki ni uhuni.
Malaika amefunguka hilo kupitia kipindi cha MamaMia ya East Africa Radio wakati anazungumzia sababu zinazofanya wasanii wa kike kuwa wachache kwenye kiwanda cha BongoFleva.
"Mimi wakati naanza muziki nilimaliza mwaka mzima bila mazungumzo na baba yangu kisa alikuwa naona kama uhuni, pili kumsimamamia msanii wa kike ni kazi kuliko mwanaume kwa sababu tunagharama nyingi ndio maana watoto wakike wanakuwa wachache kwenye muziki" ameeleza
Aidha Malaika ameendelea kusema "Tuna dhana ambayo ipo tangu zamani japo sasa hivi tunapambana nayo, iliaminishwa mtoto wa kike hawezi kufanya kitu na kipindi kile muziki ulikuwa ni wanaume wengi".