China imetangaza kwamba hakuna uwezekano wowote kuwa virusi vya corona (Covid-19) vilivujishwa kutoka kwenye maabara.
Maafisa wa China walitoa taarifa katika mkutano uliohudhuriwa na wawakilishi wa nchi 50 kuhusu utafiti unaoendelea kabla ya ripoti rasmi inayotarajiwa kutangazwa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) juu ya chanzo cha Covid-19.
Akielezea kuwa inakadiriwa virusi viliambukizwa kwa binadamu kutoka kwa popo, au vilipitishwa na popo kwa mamalia kisha kwenda kwa binadamu, Naibu Mwenyekiti wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini China Fıng Zıjian, alibaini kuwa virusi pia vinaweza kuwa vimesambazwa kupitia vyakula vilivyohifadhiwa.
Fıng alisema kuwa hakuna uwezekano wowote kwamba virusi hivyo vilivujishwa kutoka kwenye maabara.
Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje Yang Tao alisema,
"China imepambana na janga hilo kwa uwazi na wala hakukuwa na chochote cha kuficha."