Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametoa pole kwa watanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
I'm sorry to hear that @MagufuliJP, President of Tanzania, has passed away. My thoughts are with his loved ones and the people of Tanzania.— Boris Johnson (@BorisJohnson) March 17, 2021
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametoa salamu za pole kwa taifa la Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
#RDC 17.03.2021|#CitéUA
Le Chef de l'État, Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo a appris avec une grande tristesse la disparition de son homologue et frère, M. John Magufuli, Président de la Tanzanie— Présidence RDC (@Presidence_RDC) March 17, 2021
Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali na taifa la Somalia, ningependa kuwasilisha rambi rambi zetu kwa Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania kwa kumpoteza Kiongozi Rais John Magufuli. Tunalitakia taifa Zima na Serikali subra na utulivu katika kipindi hiki cha maombi na maombolezo. pic.twitter.com/cQz3rALaPt — Mohamed Farmaajo (@M_Farmaajo) March 17, 2021
Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
Expresamos nuestras sentidas condolencias al Pueblo de Tanzania por la sensible pérdida física de su Presidente, John Pombe Joseph Magufuli. Un gran abrazo fraterno y toda la solidaridad a sus familiares, amigos y hermanos de la Madre África. pic.twitter.com/jf90XYXKoy— Nicolás Maduro (@NicolasMaduro) March 18, 2021
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo Behgjet Pacolli ametoa salamu kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.
#Venezuela expresses its consternation for the death of the President of the United Republic of #Tanzania, Honorable John Pombe Joseph Magufuli. Our condolences and solidarity to his family, his government and the brother Tanzanian people. May he rest in peace! pic.twitter.com/Pu4tAWzuXi— Jorge Arreaza M (@jaarreaza) March 17, 2021
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 majira ya saa 12:00 Jioni.
Mama Samia amesema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.