Matamshi yake yanajiri baada ya the Vatican kutoa taarifa ya kukumbusha walimwengu kwamba kanisa katoliki haliwezi kubariki `ndoa za wapenzi wa jinsia moja'.
Mkutano wa mafundisho katika kanisa hilo kwa jina maarufu CDF ulidai kwamba makuhani hawawezi kwa njia yoyote kutoa baraka kama hizo kwasababu ''Mungu hawezi kubariki dhambi''.
Kanisa katoliki haliwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja
Taarifa hiyo iliidhinishwa na papa Francis , ambaye awali ametoa ishara ya kutokubaliana na wale walio na msimamo mkali katika kanisa hilo kuhusu suala la wapenzi wa jinsia moja.
''Wana haki kuwa katika familia'': Papa Francis alisema akiwaunga mkono wapenzi wa jinsia moja.
Wanachama wengi wa Muungano wa wapenzi wa jinsia moja duniani LGBT walikasirishwa na msimamo huo akiwemo Elton John.
Mwanamuziki huyo wa Uingereza alichapisha katika mtandao wake wa twitter:
"Inakuwaje Vatican haiwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja kwasababu ni dhambi na badala yake baadaye wajipatie faida kupitia uwekezaji wa mamilioni ya madola katika Rocketman, filamu inayosherehekea ndoa yangu kwa David???''.