Wakati una ujauzito wa mapacha, Mama anaweza kuongezeka uzito haraka sana kuliko akibeba Ujauzito wa Mtoto mmoja. Uchunguzi wa mara kwa mara wa Daktari unaweza kusaidia kujua ukuaji wa Mimba
Kusogea kwa Mtoto tumboni hutokea mapema sana wakati ukiwa na ujauzito wa mapacha kuliko mimba ya Mtoto mmoja
Ujauzito wa Mapacha huambatana sana na kukosa pumzi, hii ni kwasababu ya ukuaji wa mfuko wa uzazi unaobana mapafu hivyo kusababisha kuhisi kukosa hewa mara kwa mara
Nyonga kuuma ni ishara mojawapo ya ujauzito wa mapacha kwani kukua kwa mfuko wa kizazi kusio kwa kawaida husababisha nyonga kuuma kwani uzito unaongezeka na kukandamiza nyonga.