Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) imesimamisha mechi zote za ndani ya nchi kwa kipindi cha wiki mbili ili kuungana na Watanzania kuombeleza msiba wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli kilichotokea jumatano ya tarehe 17/03/2021.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF kwa umma, shirikisho hilo limeufuta mchezo wa kirafiki wa 'Taifa Stars', uliyopaswa kufanyika leo alhamis tarehe 18/03/2021 katika uwanja wa Moi Kasarani nchini Kenya kupitia tatizo hili lililoikumba Taifa,
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ipo kambini nchini Kenya kwa takribani wiki sasa na kufanikiwa kucheza mchezo moja na Harambee Stars uliyomalizika kwa kupoteza 2-1 na ule wa marudiano ulipaswa kupigwa leo,
Stars inajiwinda na michezo ya kufuzu AFCON 2022 nchini Cameroon, ambapo tarehe 25/03/2021 inatarajiwa kucheza ugenini na Equtorial Guinea na kisha kumaliza tarehe na 28/03/2021 na Libya. Stars iliyoko chini ya kocha Kim Poulsen inaonekana kuwa na mikakati mikubwa kuhakikisha inafuzu
Kwa upande wa ndani ya nchi kwa sasa ligi daraja la kwanza inaendelea pamoja na ligi ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 kutoka vilabu vya ligi kuu iliyopamba moto zitalazimika kusimama.