"Hakuna Jambo litakaloharibika"- Rais Mh. Samia

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu, amewaomba Watanzania kushikamana katika kipindi hiki na kwamba wasiwe na hofu kwani Tanzania inayo hazina nzuri ya viongozi wakiwemo waliostaafu hivyo hakuna jambo litakaloharibika.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 19, 2021, Ikulu ya Dar es Salaam nara baada ya kula kiapo cha kuwa Rais akichukuwa nafasi ya Dkt. John Magufuli, aliyetangulia mbele za haki Machi 17 mwaka huu kwa tatizo la umeme kwenye moyo.


"Niwaombe Watanzania tuwe na moyo wa subira, tujenge umoja na mshikamano, niwahakikishie kuwa tuko imara kama Taifa na sisi viongozi wenu tumejipanga vizuri, tunayo katiba ambayo nimeapa kuilinda na kuisimamia, nchi yetu inayo hazina nzuri ya uongozi iliyojengwa na viongozi waliotutangulia, niwahakikishie kuwa hakuna jambo litakaloharibika," amesema Rais Samia Suluhu


Aidha ameongeza kuwa, "Mimi nilipata bahati ya kuwa Makamu wake (Rais Magufuli) alikuwa ni kiongozi asiyechoka kufundisha kuelekeza kwa vitendo vipi anataka nchi hii iwe, amenifundisha mengi amenilea na kuniandaa vya kutosha, naweza kusema bila chembe ya shaka kuwa tumepoteza kiongozi shupavu na mwana mwema wa Bara la Afrika".


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad