Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania imechaguliwa kuwa mshindi wa vivutio vya utalii duniani na kampuni ya Tripadvisor.
Katika tuzo hizo ambazo hutolewa na kampuni hiyo inayoshushughulika na kutoa mrejesho wa mahoteli na vivutio mbalimbali duniani.
Hifadhi tatu nchini Tanzania zimeibuka kidedea kati ya hifadhi 25 zilizotajwa kwenye tuzo hizo Serengeti ikishika nafasi ya kwanza duniani Hifadhi ya Masai Mara ya nchini Kenya imeshika nafasi ya tatu huku mbuga ya wanyama Tarangire ikishika nafasi ya 14 na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12.
Akizungumza na BBC Dira ya dunia Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti na secta ya utalii nchini Tanzania na Afrika Mashariki.
Waziri wa Mali Asili na utalii nchini Tanzania Dkt Damas Ndumbaro amesema tuzo hiyo ni yenye umuhimu mkubwa kwa Serengeti
"Tuzo hii tumepata ushindi kutokana na kazi nzuri tunayo ifanya ya kuhifadhi mbuga hii maarufu ya Serengeti,lakini pia na huduma bora ukiwa Serengeti unaweza ukaona Wanyama kwa urahisi na vizuri zaidi"
Serengeti pekee kwa mwaka hupokea wastani wa wageni laki tatu na nusu hadi laki tano ambao huja kushudia maajabu yaliyoko kwenye eneo hili ambalo ni urithi wa dunia ikiwa na na ukubwa wa kilomita za mraba 14750 kila mwaka hushuhudia mamilioni nyumbu ambao wanahama kutoka hifadhi Masai mara nchini Kenya ambayo nayo kwenye tuzo hizi imeshika nafasi ya tatu. Utalii kama zilivyo sekta nyingine kote duniani umeathirika na uwepo wa maradhi ya Covid-19.
Mamlaka ndani ya hifadhi zimejiwekea mkakati maalumu kuhakisha wageni wanakuwa salama muda wote wawapo hifadhini ikiwa ni Pamoja na kuweka kituo cha ukusanyaji wa sampuli, kwa ajili ya upimaji wa virusi vya corona ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti mamlaka zinasema lengo ni kuharakisha upimaji lakini pia kuwapatia muda wakutosha wageni kuwa hifadhini.