Kanisa katoliki haliwezi kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja






Kanisa katoliki halina uwezo wa kubariki ndoa za wapenzi wa jinsia moja, afisi ya mafundisho mjini Vatican imesema.
Haiwezekani kwa Mungu kubariki dhambi, Afisi inayokutana kutoa mafundisho imesema siku ya Jumatatu.

Hatahivyo afisi ya mkutano huo ilitambua kwamba kuna mambo mazuri katika mahusiano ya wapenzi wa jinsia moja.

Mwezi Oktoba, Papa Francis alisema katika makala moja kwamba alifikiria kwamba ndoa za wapenzi wa jinsia moja zinapaswa kuhalalishwa.

Papa Francis anaonyesha kuunga mkono vyama vya wapenzi wa jinsia moja, Katika Kanisa Katoliki, baraka hutolewa na kuhani au mhudumu mwingine kwa jina la Kanisa.

Siku ya Jumatatu papa Francis aliidhinisha jibu la mkutano wa mafundisho, akisema kwamba sio njia ya kuwabagua, badala yake ni ukweli wa lituriki.

"Baadhi ya parokia katika miezi ya hivi karibuni, ikiwemo Ujerumani na Marekani zimeanza kuwabariki wapenzi wa jinsia moja kama njia ya kuwakaribisha wakatoliki wa penzi wa jinsia moja katika kanisa hilo, Kitengi cha habri cha reuters .

Jibu hilo la CDF lilitokana na jibu kutoka kwa swali lililoulizwa.

Je kanisa hilo lina uwezo kutoa baraka kwa ndoa za wapenzi wa jinsia moja? Lilijibu hapana.

Mkutano wa mafundisho hayo ulisema kwamba ndoa kati ya wanaume na wanawake ni sakramento na hivyobasi baraka haziwezi kupewa wapenzi wa jinsia.

Kwasababu hiyo, sio makosa kutoa baraka kuhusu mahusiano, au ushirikiano m hata yalio thabiti ambayo uhusisha vitendo vinavyohusisha tendo la ndoa njeya ndoa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad