Katambi Awaponda Chadema “Huwezi Kujenga Ofisi, Utaweza Nchi?”

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Group na Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo (kulia) akimpokea Naibu Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Patrobas Katambi.

NAIBU Waziri wa nchi, ofisi ya waziri mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu, Patrobas Katambi, leo Machi 10, 2021 ametembelea ofisi za Global Group na kufanya mahojiano kwenye studio za Global Radio, kuhusiana na masuala mbalimbali yanayuhusu serikali kwenye wizara yake.

 

Katambi amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano na Kipindi Maalum cha Global Radio leo Jumatano, Machi 10, 2021 ambapo ameongeza kuwa katika maisha yake amekuwa nikijitoa mhanga, si tu kwa ajili ya kujitoa bali ni kutokana na maono ambayo Mwenyezi mungu amekuwa akimpa.

 


“Wakati nilikiwa Chadema nilikuwa nikitoa chambo, nilikuwa tayari kutukanwa na kugandamizwa lakini kutetea misingi tuliyoiamini. Kuingia upinzani sikutoka barabarani, si kwamba walinisaidia, tumesaidiana, harakati nyingi tulizifanya. Kabla ya hapo nilikuwa CCM.

 

“Katika chama kile niliwambia kwamba kabla hujatoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako toa la kwako kwanza, kwenye masuala ya fedha haiko sawa, uongozi na demokrasia haiko sawa, uchaguzi wa ndani ya chama mnaumizana, vinakaa vikao vya kinafiki kuumiza wengine.

“Kama wewe unayetaka kupewa nchi ambaye BoT itakuwa chini yako na taasisi nyingine za fedha lakini matumizi ya pesa kwenye chama chako huwezi. Nikawa ninaargue sana lakini nikaonekana kama ninalalamika.

 

“Kuna wakati tulifika hali haikuwa nzuri sana, kuanzia uchumi na huduma kwa jamii. Tukafanikiwa kuingiza watu wengi Bungeni tukatawala maeneo kama Ubungo na Umeya jiji zima la Dar, Jimbo la Hai na maeneo mengine, lakini ukiangalia kilichofanyika hakuna.



 

“Kawe, Hai, Ubungo na maeneo mengine ya Chadema yalitakiwa yawe ya mfano, nikawaambia huu si wakati wa kufanya haya tunayoyafanya, tunapaswa kuonyesha utofauti na washindani wetu katika ukweli, uadilifu, uchapakazi na vitu vionekane.

“Mpaka siku nasema basi (Chadema), nilishambuliwa sana kwa sababu ya misimamo yangu, nilitengenezewa mazingira nikaonekana kama kondoo kwenye kundi la simba, kwa hiyo huwezi kunyosha kidole ukazungumza. Sababu ya kile nilichokiamini na msimamo yangu.




“Kuna watu walikuwa wanahongwa safari lakini mimi sikuwa tayari, unatengenezewa mazingira magumu ya kuua ndoto yako, nikaona bora nikawaachia chama chao, kuna vijana wengi wameumizwa sana, watoto wa kike, pia wapo niliowasaidia na leo wamekuwa wabunge.



“Nilikabidhi kwa maandishi pesa takribani Tsh 10m na mali zote za chama, gari nililotafuta kwa ajili ya vijana naamini sasa hivi hawana. Ningekuwa nimenunuliwa ama niatamaa nisingekabidhi hizo mali, nikarudi nyumbani kujitafakari, na mama yangu alikuwa mgonjwa sana.

 

“Kama ingekuwa usaliti basi nilisaliti wanafiki kwa ajili ya maslahi ya vijana na taifa lao, mission tuliyokuwa nayo ni kuwasaidia Watanzania, kuwa waaminifu na kufanya kazi kwa uadilifu kwa kufuata katiba ya chama, hayanyiki, nimeamua kuondoka, nani msaliti?




“Kama nilishindwa uchaguzi mwaka 2015 na ndio ilikuwa sababu kwa nini nisiondokea mwaka 2016? CCM sasa kimejisafisha, kimekuwa kama ndo chama cha upinzani, yale yote tuliyokuwa tukiyapigia kelele ndo yanafanyiwa kazi, madiniu, uadilifu, rasilimali za nchi na mengine.

 

“Lengo letu ni kujenga nchi, vyama mbalimbali, tunatoka maeneo mbalimbali lakini Taifa letu ni moja, kila mtu anao wajibu anao wajibu wa kujenga Taifa. Huu wadhifa niliyoupata sio kwamba kwa sababu mimi ni bora sana kuliko wengine, bali huu ni mpango wa Mungu. Wajibu wangu ni kwenda kubadilisha maisha ya vijana. Mwaka 2015, Mhe. Rais aliahidi ajira milioni 8, zikapatikana ajira zaidi ya milioni 11.

 

“Mhe. Rais aliagiza pesa zinazokusanywa kwenye Halmashauri, 4% iende kwa vijana, 4% iende kwa wanawake na 2% iende kwa wenye walemavu, mpaka sasa Serikali inawadai zaidi vijana mabilioni ya pesa ambayo imepeleka kule ili ziweze kuwasaidia kujiendeleza.




“Nimefikiria badala ya kuwapa pesa, vijana tuwape vifaa nusu na nusu tuwape pesa, mfano wanataka kuanzisha studio tutawalipia pango, kuwanunulia vifaa na nusu tutawapa pesa ya uendeshaji, hata wakishindwa vifaa vitaidia wengine, ukiwapa pesa tu zinaishia mfukoni.

 

“Tunaweza kuona namna kwa sababu vijana wengi hawana assets za kuweka bondi, hata cheti chake cha digrii anaweza kuweka bondi kama anavyokopeshwa na Bodi ya Mikopo, akapewa pesa akaanza biashara. Tuondoe dhana ya kwamba kila mtu ataajiriwa.



“Taifa litakuwa litakuwa na hatari sana kama litakuwa halina ajira wala kazi. Kazi zipo nyingi sana hazihitaji elimu, inatakiwa uwe na maarifa na ujuzi, watu wengi waliofanmikiwa ni wanaofanya kazi na si ajira. Ukiwa na ajira huwezi kufikia ndoto za kuwa tajiri.



“Ajira unakuwa mtumishi, maana yake unakuwa mtumwa. Nafasi hizi tunazozitumikia ni kwa neema tu ya Rais Magufuli, hatupaswi kuwa wanafiki lazima tuwaambie vijana ukweli.

 

“Kuna makampuni unakuta wapo wafanyakazi wa kigeni 32 na Watanzania 700, lakini ukichukua mishahara ya Watanzania wote ukaijumlisha hawawafikii wageni, huu ni utoroshaji wa fedha wanaenda kuwekeza kwao, nyadhifa zote za juu kwenye kampuni hizo wanapewa wageni.



“Unakuta kifaa cha mgodini kinanunuliwa Sh 5m Tanzania lakini wanakwenda kununua nje kwa Sh 7m, wamepigwa Sh 2m, pesa ile inatoka kwenye mzunguko wa fedha wa Tanzania inaenda kufanya kazi kule, sasa mimi nasema kabla sijatumbuliwa wengine watakuwa wameshasagika.



“Lazima mwaka huu tukae kikao cha ‘Utatu Mtakatifu’ yaani Serikali, Waajiri na Wafanyakazi, vyama vya wafanyakazi na waajiri wana siri nzito kila mmoja, tunataka tuzijue, Waziri wa Elimu naye awepo huenda vyuo vinatoa vyeti bila kujua soko la ajira linataka nini,” Mhe. Patrobas Katambi.




Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad