Kauli ya Zitto kabla ya Magufuli kuzikwa

 


Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, leo ametoa waraka wake wa kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli, ambapo pamoja na mambo mengine amemsifu kwa namna ambavyo alijitahidi kujenga nchi kitendo ambacho kila mmoja anamsifu.

 


Waraka huo ameuandika na kuuweka kwenye ukurasa wake wa Twitter hii leo Machi 26, 2021, na kueleza kuwa imemchukua karibu wiki nzima kuandika japo kidogo neno la kumuaga Hayati Magufuli, huku akidai kuwa imemchukua muda kuandika kwa sababu amechoka kuandika Tanzia sababu ya vifo vingi vilivyotokea mapema mwaka huu.


"Watu ambao nilikuwa nawaona kama wazee wangu, Walimu wangu na washauri wangu kama Profesa Benno Ndulu, walitangulia mbele ya haki wiki chache kabla yako, nawe pia ulipoteza mtu wako wa karibu katika kazi Balozi John Kijazi, mwezi mmoja kabla ya umauti kukufika, hakika robo ya kwanza ya mwaka 2021 imekuwa mtihani mkubwa kwa nchi yetu," ameandika Zitto


Aidha Zitto ameongeza kuwa, "Nimepata nguvu leo kukuaga Rais kwa sababu licha ya machungu mengi moyoni mwangu nina kumbukumbu nzuri nawe, nilipopata ajali wakati wa kampeni ulikuwa tayari kutoa kila msaada ili niweze kupona, ulinipa faraja nikiwa hospitalini kwa kunipigia simu mara kwa mara kunijulia hali, ninaamini ulikuwa unaniombea kupona ili kuendelea na kazi zangu".


Mbali na hayo Zitto amesema kuwa, "Rais John Pombe Magufuli, wakati tunakuhifadhi leo katika nyumba yako ya milele kijijini kwako Chato mkoani Geita, ninakuombea kwa Mungu ailaze roho yako mahala pema. Mungu akuepushe na  adhabu ya kaburi. Mungu akusamehe dhambi zako zote. Pumzika kwa Amani"

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad