Kenya yaipa siku 14 UNHCR kuzifunga kambi kubwa mbili za wakimbizi




Kenya imetangaza mipango ya kuzifunga kabisa kambi mbili za wakimbizi ambazo ni makaazi ya zaidi ya watu 400,000,ikisema hakuna tena nafasi ya kufanyika mazungumzo huko baadae kuhusiana na kambi hizo.



Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imeliagiza shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughukilia wakimbizi, UNHCR kuandaa mpango ndani ya siku 14 zijazo wa kufunga kambi za wakimbizi za Kakuma iliyoko kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo na Daadab iliyoko Mashariki karibu na mpaka wa Somalia.

Kambi ya Kakuma ni makaazi ya kiasi watu 190,000 wengi wao ni wakimbizi kutoka Sudan Kusini,wakati Daadab ina watu takriban robo milioni wengi ni wasomali waliovuka mpaka kukimbilia Kenya kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka 1991.

Kenya imewahi kutishia mara mbili kufunga kambi hizo mwaka 2019 na 2016 lakini sasa waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang ametowa taarifa kupitia ujumbe wa twitta akisema hakuna tena nafasi ya mazungumzo zaidi juu ya suala hilo.

Kenya inasema kambi ya Daadab inatumiwa na kundi la wanamgambo wa itikadi kali wa al-Shabaab kutoa mafunzo na ni kitisho cha usalama wa taifa hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad