Kenya yapokea shehena ya chanjo ya Covid-19

 


Shehena ya chanjo ya Covid-19, dozi milioni 1.02 za Oxford-AstraZeneca imetua katika uwanja wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi nchini Kenya, ikitokea taifa la India.

 

Chanjo hizo zilizofika usiku wa kuamkia leo Machi 3, 2021, ni shehena ya kwanza kati ya chanjo milioni 3.56 zitakazopelekwa Kenya.


Aidha, taarifa kutoka Kenya zimeeleza kuwa chanjo hiyo itaanza kutolewa kesho kwa Wahudumu wa Afya, Walimu na walio na magonjwa mbalimbali.  


Kwa upande wa viongozi wa nchi ambao ni Rais Uhuru Kenyatta, Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wanatarajiwa kupewa chanjo hiyo siku ya Jumamosi, Machi 6, 2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad