Mamlaka ya Kilimo na Chakula ya Kenya imedai uchunguzi umebaini kuwa mahindi yanayoingia kutoka Tanzania na Uganda sio salama kwa matumizi ya binadamu
Imedai kuwa, mahindi hayo yana kiwango kikubwa cha sumu hasa aflatoxins na fumonisins ambazo zinajulikana kusababisha Saratani
Mamlaka hiyo imedai, Sumu hizo zimesababisha vifo vya Wakenya wengi kwa miaka, hali iliyosababisha wachukue hatua ya kuacha kupokea mahindi kutoka Tanzania na Uganda
Aidha, imesema wataendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na nchi wanazoshirikiana nazo kibiashara na wanasubiri kuona washikadau wakilizungumzia tatizo hilo