Kikosi cha anga Uturuki kimeshambulia eneo la Kikurdi






Kikosi cha anga cha jeshi la Uturuki kimefanya mashambulizi yake ya kwanza katika miezi 17 dhidi ya eneo la kaskazini mwa Syria linaloshikiliwa na wanamgambo wa Kikurdi Jumamosi usiku. 


Kulingana na shirika la uangalizi wa haki za binaadam la Syria SOHR, ndege ya kivita ya Uturuki imeshambulia maeneo ya vikosi vya jeshi la demokrasia la Syria (SDF) katika kijiji cha Saida huko Ain Issa vijijini na kusababisha milipuko mikubwa. 



Huo ndiyo ulikuwa uvamizi wa kwanza tangu kampeni iliyopewa jina la "Operation Peace Spring" iliyoanzishwa Oktoba 2019 na Ankara na washirika wake wa Syria dhidi ya SDF kaskazini mwa Syria. 



Mashambulizi hayo yamekuja siku ambayo imeshuhudia mapigano ya vurugu na mashambulizi makali ya roketi katika wilaya ya Ain Issa kati ya vikosi vya SDF na vikundi vinavyoungwa mkono na Uturuki.



Mkurugenzi wa SOHR, Rami Abdul Rahman ameiambia AFP kuwa mapigano kati ya pande hizo mbili yamedumu kwa saa 24, na kwamba vikosi vya Uturuki vimepata ugumu kusonga mbele baada ya SDF kuharibu kifaru chake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad