Kikosi cha timu ya Simba chawasilia salama jijini Khartoum Sudan


MSAFARA wa wachezaji 25 wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes umewasilia salama  jijini ,Khartoum, Sudan.

Kikosi kilikwea pipa jana Machi 3 na kilipitia Addis Ababa, Ethiopia usiku wa kuamkia leo kilianza safari kuibukia Sudan ambapo kimeweza kufika salama.


Orodha ya nyota hao ambao ni wachezaji 25 hii hapa:-


Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Shomari Kapombe, Joash Onyango, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Jonas Mkude, Rarry Bwalya, Mzamiru Yassin.


Luis Miquissone, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajibu, Clatous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere, John Bocco.


Miraji Athuman, Kope Mugalu, Peter Muduhwa, Tadeo Lwanga, Kenedy Juma na David Kameta. 


Machi 6 kinatarajiwa kuwa na mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Merrikh ambayo ipo nafasi ya nne ikiwa haijaambulia pointi.


Hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wapinzani wao wakisaka pointi tatu mbele ya Simba ambayo nayo inahitaji pointi hizo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad