Kocha AS Vita Aiita Yanga Mezani





KOCHA Msaidizi wa AS Vita Club ya DR Congo, Raoul Shungu, amesema kuwa yupo tayari kuisikiliza ofa ya Yanga kama watahitaji huduma yake.

 

Yanga, Jumanne ya Machi 3, ilimtambulisha Juma Mwambusi kuwa kocha wa WACHEZAJIwa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jemba Ulaya’ na Adolf Rishard wamesema kuwa kama klabu hiyo inataka mafanikio msimu huu, ni vema wamuache kocha wa muda wa timu hiyo, Juma Mwambusi amalize msimu akiwa anakiongoza kikosi hicho.

 

Hoja kubwa ya wakongwe hao ambao ni walimu wa soka kwa sasa wanadai kuwa Mwambusi anaifahamu Yanga vizuri kwa kuwa siyo mara yake ya kwanza anakaa kwenye benchi la timu hiyo, hivyo uzoefu wake utasaidia kurekebisha makosa na kurudisha makali ya timu hiyo ambayo bado ipo kileleni.



Malima alisema: “Kwanza naupongeza uongozi wa Yanga kwa kumrudisha Mwambusi kwenye benchi, kwa sababu ni kocha ambaye anaifahamu vizuri timu kwa sababu ameshakaa hapo kwa mara kadhaa, hivyo nadhani kama wangempa timu aende nayo hadi mwisho wa msimu anaweza akaipa mafanikio.

 

Kwa upande wa Adolf ambaye ni kocha wa zamani wa Tanzania Prisons, alisema:

“Ni sawa kumrudisha Mwambusi kwa sababu ni kocha ambaye ana sifa na uwezo mkubwa kwa hapa Tanzania lakini kubwa zaidi amekaa na ile timu mwanzoni mwa msimu, anawajua wachezaji wote, hivyo naona kama wangemuacha amalize msimu ingekuwa kitu bora zaidi.”

 

Mwambusi amerejeshwa Yanga, mara baada ya timu hiyo kutimua benchi lote la ufundi na yeye amekabidhiwa timu mpaka pale kocha mpya atakapopatikana.

 

Mwambusi aliondoka kwenye timu hiyo kwa matatizo ya kiafya na nafasi yake ilichukuliwa na Nizar Khalfan ambaye naye ametimuliwa.

 

VITA ya kisasi inapigwa leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Chuo cha Mzumbe ambapo timu ya Via Veterani itakuwa kwenye kibarua kizito mbele ya kikosi cha VIA Vijana.Michezo miwili iliyopita na kuzikutanisha timu hizo iliisha kwa kila upande kuibuka na ushindi kwenye mchezo mmoja na kupoteza mara moja.

 

Via Veterani waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 huku mchezo wa pili, Via Vijana wakiwafunga Veterani mabao 4-2.

 

Nahodha wa kikosi cha Via Veterani, Ammy J alisema: “Kikosi chetu kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wetu wa kesho (leo) Ijumaa dhidi ya Via Vijana, tunaingia katika mchezo huu tukiwa na kumbukumbu mbaya ya muda wa timu hiyo lakini bado wanatafuta kocha mkuu wa kuja kuziba nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Cedric Kaze.

 

Shungu, mwenye uraia wa DRC, aliwahi kuwa kocha mkuu wa Yanga na kuipa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 1998/99 ambapo mwaka 2001 aliondoka klabuni hapo na nafasi yake ilichukuliwa na mzawa Boniface Mkwasa.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha huyo alisema kuwa yupo tayari kuisikiliza ofa ya Yanga kama itahitaji huduma aifundishe timu hiyo ambayo aliwahi kuifundisha zamani.

 

“Nimesikia kuwa aliyekuwa kocha mkuu kwa sasa hayupo, sijawasiliana na kiongozi yeyote wa Yanga juu ya kuwa kocha wao lakini kama watakuwa wananihitaji basi nitasikiliza ofa yao ipoje kwangu.“

 

Nimeshawahi kuwa kocha wa Yanga, mpira wa Tanzania naufahamu vizuri na changamoto zake, nafurahi niliishi vizuri wakati nipo Tanzania, muda mwingine napaona kama nyumbani,” alisema kocha huyo.

Stori: Marco Mzumbe,Dar es Salaam

 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad