KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema kupoteza pointi mbili mbele ya Prisons baada ya sare ya 1-1 Jumatano iliyopita, haijaondoa mipango ya timu hiyo ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa na michezo mingi mkononi.
Mfaransa huyo ameongeza kwamba, anachokifanya kwa sasa ni kuwajenga wache-zaji wake na kuongea nao ili wafanye vizuri katika mechi zijazo.
Gomes ameliambia Spoti Xtra, kuwa: “Kile ambacho kimepita kwa sasa siyo ishu, kwa sababu tunaangalia nini ambacho kilichopo mbele yetu.
Tulitoka sare na Prisons, lakini haiondoi chochote katika kupigania nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zinazokuja.“Tuna mechi mkononi ambazo tunatakiwa kufanya vizuri tofauti na ilivyokuwa katika mechi iliyopita.
Muhimu kubadilisha makosa ambayo tuliyafanya kwa ajili ya kupata matokeo mazuri,” alimaliza Gomes.Hivi sasa vinara wa ligi hiyo ni Yanga wenye pointi 50 baada ya kucheza mechi 23, Simba inafuatia ikiwa na pointi 46 ikicheza mechi 20.