Kocha wa Yanga amtaja anayeihujumu timu hiyo



 
Aliyekuwa kocha wa magolikipa wa klabu ya Yanga, Mrundi, VladmirNiyonkuru amefunguka mambo mengi baada ya benchi la ufundi la klabu hiyo kuvunjwa siku ya jana ya tarehe 8 Machi 2021 kufuatia mwenendo wa matokeo yasiyoridhisha kwa viongozi na wanachama wa timu hiyo.

Aliyekuwa kocha wa Makipa wa klabu ya Yanga, Vladmiri Niyonkuru
Akizungumzia namna benchi hilo lilivyoondolewa, Niyonkuru ameiambia East Africa redio kupitia kipindi cha “Kipenga Xtra' “Hawajatuitisha sisi kwa pamoja, kila mtu aliitwa kivyake. Mimi wakaniambia wakiangalia timu inavyoenda kwa sasa, tumeamua tusitishe mkataba na wewe. Mimi sikuuliiza zaidi sababu ila iliwapa mkono na kushukuru na nikaondoka zangu”.

“Nadhani kesho tutakaa kuzungumzia kuhusu kumalizana kimkataba, maana ndiyo kwanza nimefika Dar kutokea Arusha”.

Baada ya kusema hayo, kocha huyo aliyejiunga na Yanga mwezi Agosti mwaka jana, aligusia juu ya moja ya kiongozi anayeiharibu tiu hiyo ikiwemo kuingiliwa kwenye majukumu yao kama benchi la ufundi.

“Mimi siwezi kumtaja huyo tu lakini yupo, alijaribu kufanya hivyo. Nawaambia wanayanga na mashabiki wake wakiwa wanachagua viongozi, wachague viongozi walio sahihi”. Maelezo yake hayo yaliendelea na hata kukiri kuwa kuna kiongozi anayeiharibu timu huyo ila hayupo tayari kumtaja.

“Nakwambia kuna kitu, kuna kitu kipo nyumba na kuna mtu ana haribu hiyo timu ninyi waandishi mfanye uchunguzi mtajua”.

Maneno hayo yamezidi kuwaaminisha wadau wa soka nchini kuwa, kwenye  Uongozi wa klabu ya Yanga kuna mapungufu mengi baina ya Viongozi wa juu jambo linalochangia timu hiyo kukosa utulivu hivi sasa na kupelekea kupata matokeo mabaya.
 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad