Korea Kaskazini yafyatua makombora ya masafa marefu




Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa marefu ndani ya bahari ya Japan, zimesema Marekani na Japan- likiwa ni jaribio la kwanza la aina hiyo tangu Joe Biden awe rais wa Marekani.



Pyongyang ilizuiwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu, ambayo yanaangaliwa kama silaha za kutisha, chini ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Japan imesema kifusi kimeanguka ndani ya eneo lake la maji. Hii inakuja siku chache tu baada ya Korea Kaskazini kufyatua makombora yasiyo ya Bahari ya Manjano.

Waziri mkuu wa Japan Yoshihide Suga amesema Alhamisi kwamba majaribio hayo yanaleta tisho kwa usalama na amani kwa nchi yake pamoja na kanda hiyo nzima.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa wakuu wa jeshi nchini Korea Kusini awali ilisema makombora hayo yalirushwa kutoka katika “kitu ambacho hakijatambulika “.

Bw Biden bado hajatoa taarifa rasmi kuhusu jaribio la hivi karibuni la Korea Kaskazini. Siku ya Jumanne alipuuza ufyatuaji wa makombora yasiyo ya masafa marefu yaliyorushwa mwishoni mwa juma, akisema kuwa Marekani haikuchukulia jaribio hilo kama uchokozi.

Makombora hayo ya masafa marefu yalidhaniwa kuwa ya kutumia roketi ambayo kwa kawaida hulenga eneo fulani, ambayo hayajapigwa marufuku na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Jaribio hili lina maana gani?
Hili ni jambo kubwa sana kwa Marekani na washirika wake

Jaribio la mwishoni mwa juma la makombora ya masafa mafupi linaweza kupuuzwa. Lakini jaribio hili ni ukiukaji wa wazi wa vikwazo vya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Kwa kusema hivyo, mtangulizi wa Bw Biden Donald Trump hakutaka maswali yoyote kuhusu jaribio la silaha sawa na hizo mwaka 2019.

Mkataba baina ya Bw Trump na Kim Jong-un uliofikiwa nchini Singapore mwaka 2018 ulikuwa kwamba Pyongyang haitajaribu makombora ya masafa marefu au silaha za nyuklia.

Wakati ule, Ikulu ya White House haikujihusisha na majaribio madogo zaidi ya makombora. Lakini maafisa wa Bw Biden ndio wametoka tu nchini Japan na Korea Kusini, na kuahidi kuwa “Marekani imerejea” na inawaunga mkono washirika wake.

Labda sasa, utawala Biden, utatakiwa kutoa tamko kuhusu jaribio la silaha ambazo zinatishia marafiki zake Kaskazini mwa Asia. Washington itatambua kuwa Pyongyang ina silaha kubwa katika gala lake ambazo haijazifanyia majaribio tangu mwaka 2017.

North Korea imetengwa kwa mwaka mmoja. Hata iliamua kukata biashara zake nyingi na mshirika wake mkuu China kutokana na janga la Covid-19 , na uchumi wake unasemekana kuwa katika hali mbaya.

Sasa wakati ikionekana kurejesha majaribio yake ya silaha, wengi wanashangaa ni kwa kiwango gani anachotaka kukifikia Bw Kim Jong-un ili kuweza kuutishia utawala wa Marekani.

Majaribio haya yanafanyika huku utawala wa Biden ukiendelea kujaribu kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na Korea Kaskazini.

Pyongyang bado haijatambua kuwa Bw Biden sasa yuko mamlakani, nan chi mbili bado ziko katika uhasama unaojhusu mipango ya Korea Kaskazini ya makombora ya ballistic na silaha za nyuklia.

Je Korea Kaskazini ina silaha za aina gani?
Kwa sasa jambo ambalo maafisa wa White House wanaliangazia pamoja na washirika wao ni tathmini inayosubiriwa kuhusu sera ya Korea Kaskazini.

Miongo ya vikwazo na mikutano mitatu baina ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na wa Korea kaskazini Kim Jong-un imeshindwa kuizuia Pyongyang.

Wakati huo huo mapema mwezi huu, Marekani ilimpokea raia wa kwanza wa Korea Kaskazini katika mahabusu yake Mun Chol Myung ambayer aliletwa kutoka Maysia.

Bw Mun ni mfanyabiashara anayeshutumiwa kwa makosa ya utakatishaji wa fedha kupitia mfumo wa fedha ya Marekani kutoa bidhaa za anasa katika Korea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad