Korea Kaskazini imesema itapuuza pendekezo la Marekani kukaa katika meza ya mazungumzo hadi pale itakapofuta sera yake ya kikatili dhidi ya utawala wa Pyongyang.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui, saa chache kabla waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken na mwenzake wa ulinzi Lloyd Austin kukutana na wenzao wa Korea Kusini mjini Seoul.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kutuwama juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na ni ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano. Choe aidha amesema hakuna haja ya kujibu maombi ya Marekani kuhusu mazungumzo.
Amekosoa mazoezi ya kijeshi ya mwezi huu akisema Marekani imeanza waziwazi mazoezi ya kijeshi za kichokozi kuilenga Korea Kaskazini.